Skip to content
Advertisements

Wolper awatolea povu wanaofatilia mapenzi yake

DIVA kutoka kiwanda cha Bongo Muvi ambaye kwa sasa amejikita zaidi kwenye biashara ya duka la nguo, Jacqueline Wolper, ametoa kichambo chenye uzito wa ‘Semi Trela’ kwa wale wote wenye tabia ya kumsakama ‘baby’ wake mpya mwanamitindo anayeitwa Brown. 

Wolper ambaye tangu athibitishe kuwa yu mapenzini na mwanamitindo huyo, baadhi ya mashabiki wake hawajawahi kumuacha salama kutokana na kumtupia maneno kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na umri wa kijana huyo kuwa ni mdogo haufanani naye yaani ‘Kibenteni’. 
Unaambiwa hata punda akikubeba kwa muda mrefu ikafika muda akachoka anakubwaga tu, na hicho ndicho kilichotokea kwa Mrz Brown, maji yalivyomfika shingoni akapita taratibu kwenye mahakama ya mastaa Instagram na kuandika ujumbe ufuatao: 
“Hivi ni nani asiyekuwa na furaha Instagram, kila mtu hujitia mapenzi mazuri, maisha mazuri, hakuna ugomvi ndani ya nyumba wakati in reality watu wanalia kimyakimya tunawachora. Wengine wanapigika wee bila kusahau mikopo kibao mpaka usiku wanaota wanakimbizana na marejesho lakini wakija Insta wanajitia wao eti wao ni wakamilifu huku wanakufa na tai shingoni tena kwa kuongea uongo. 
“Siyo lazima maisha yako uyaweke Insta, pia hakuna ulazima wa kudanganya ukweli wakati mambo yenu yako hadharani, mbona tunajuana mjini hapa. 
Sasa naomba niongee kwa sauti na nieleweke, nimeamua kuwa open book, haya ndiyo maisha niliyoyachagua mimi Jacky, bila kusahau nimeamua kuishi maisha yangu na kujipa furaha bila kujali kingine chochote. 
“Sasa nyie mnaosema huyu hafai hebu nionyesheni mabwana zenu wanaofaa, na mbona mnaocomment wengi wenzangu tu ila ndiyo mnalinda status, wengine mnajikongoja ndani hata cha maana hampewi mnawafichia siri mabwana zenu kulinda heshima mtakufa. 
“Na bado wanaume zenu wanawasaliti pia tunajua tena wanawasaliti huku wanawaongelea vibaya, haya maisha tunafanana tu tofauti yangu nimeweka wazi, tena huenda yangu ni bora, haya nyie mnaosema huyu mdogo mkisikia natoka na baba zenu wazazi mtapenda kweli, nipeni mabwana zenu basi walio wakamilifu tushee. 
“Kiufupi wote mliyofurahi post za usiku nilikuwa nataka kujua ushambenga wenu na uzushi wenu mtazusha nini na kweli mmeyazua nimezoom comment zenu nimejua maombi yenu, pia niwape tuu big up kwa mafunzo mliyosomea. 
“Na kama mngekuwa mnajua kazi kama umbea na roho mbaya tungekuwa madoni, nikiachwa pia mtajua maana mi siyo wa kwanza wala wa mwisho duniani na sijuagi kuficha, wengine hata mama zenu waliachwa ila mko insta kung’ang’ania ya watu. 
“Usiforce tufanane haya ni maisha yangu nitayaendesha vile ninavyojisikia sisi bado tupo sana tu, kwa sasa jamani, huyu asiyefaa ndiye ninayempenda, ili kuepusha foleni maana anayefaa itakuwa stress jamani, hafai wa kwangu, mdogo wa kwangu, hana hadhi yangu wa kwangu mimi ndiye ninajua ninachokitaka maana haya ni maisha yangu. 
“Hata wa mwanzo si mlisema hana hadhi mbona mnamuona wa maana sasa! Kila mtu ashike lake jamani kwa huyu Nimeshindikana”

Advertisements
%d bloggers like this: