Skip to content
Advertisements

HUYU NDIO NYOKA MWENYE KASI ZAIDI NA MWENYE SUMU KALI ZAIDI DUNIANI

Leo nataka tufahamishane kuhusu nyoka huyu hatari kwa sisi waswahili tunamuita KOBOKO lakini kwa lugha ya Kingereza huitwa Black Mamba.
MAMBAS ni aina ya nyoka wakali wapatikanao ktk dunia ya leo. Ni nyoka wenye sumu kali na wenye kasi ktk mwendo na wana sifa ya kutaga mayai (oviparous).

Kuna aina mbili za mambas :

1. GREEN MAMBAS.

2. BLACK MAMBAS.
Green mamba wana sumu aina ya NEUROTOXIC na HAEMOTOXIC. Wanaishi miaka 12 hadi 14 (makadirio kulingana na takwimu za sayansi) wanataga mayai na kuanguliwa kwa siku 80 hadi 90.
BLACK MAMBA pia wanauwezo wa kupanda miti wakati wakitafuta chalula na wanaurefu kati ya sentimita 220 hadi 320. Ni kati ya nyoka wenye sumu kali wapatikanao Afrika. Wanataga mayai kati ya 12 na 18,na kuangua kati ya siku 80 hadi tisini.

Mambas ni nyoka wakali na wenye kung’ata zaidi ya mara moja kwa sababu meno yao hayang’ooki wakti wakigonga kitu. Meno yanayong’ooka kwa nyoka yanaitwa FRONT FANGED MOVABLE na yasiyong’ooka yanaitwa FRONT FANGED FIXED.

BLACK MAMBA.

Black mamba ni moja ya nyoka hatari sana katika dunia. Nyoka hawa hupatikana katika sehemu Mashariki na Kusini mwa Afrika. Black mamba anaweza kuishi katika aina mbalimbali za mazingira: savanna, mabwawa, misitu na maeneo ya miamba. 
Makazi yoyote ambayo hutoa joto na unyevunyevu ni sehemu nzuri ya kuishi Black Mamba. Kutokana na uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa kilimo, makutano kati ya Black Mamba na binadamu yameongezeka zaidi.
1- Black mambas ni nyoka mwenye sifa ya urefu anaweza kufikia miguu 14 urefu na Kilo 1.58757 katika uzito.

2- Black mamba ana mwili mwembamba wenye kufunikwa na ngozi yenye magamba kama ilivyo kwa nyoka wa jamii nyingine, Pamoja na wao kujulikana kwa kiingereza kama Black mambas lakini wengi hawana rangi nyeusi katika ngozi na rangi ya mwili inategemea makazi yao na inaweza kuwa ya kijani, kijivu au njano.


3- Black mamba ni jina lake kwa sababu sehemu ya ndani ya vinywa vyao ni nyeusi kabisa. Black mamba huonyesha kinywa chake cheusi wakati anakabiliwa na hatari.


4- Nyoka huyu huanza kutanua shingo yake lakini sio kama afanyavyo COBRA na hutoa sauti kama ile ya tairi likiwa inatoka upepo na hii ni ishara nyingine kwamba kiumbe hutayari shambulio.

Ukiona ameonyesha moja ya hizo ishara unashauriwa usifanye chochote kwasababu kwa kasi aliyonayo hutaweza kumuwahi kifupi tulia mpaka hasira zishuke na ajiondokee, narudia usithubutu kujifanya unafurukuta matendo yako hayatawahi tendo lake.
5- Ingawa nyoka huyu amebeba sifa ya kuwa nyoka mjeuri na mkali sana, lakini na yeye hujaribu kutoroka kabla mashambulizi lakini hushambulia kwa ukatiri sana ikibidi. Kumbuka kwa mtulivu ukikutana nae.
6- Sasa upande wa sumu hapa ndipo patamu Black mamba ana aina mbili ya sumu zinazozalishwa katika mwili wake moja ni huitwa Neuro – hii huathiri mfumo wa neva na nyingine ni Cardio-toxin hii huathiri mfumo wa moyo na sumu hizi zinaweza huua binadamu chini ya dakika 20. Pia imethibitika kuwa matone mawili ya sumu yake inaweza kuua.
7-Black mamba anatumia sumu kuwinda aina mbalimbali za ndege na wanyama wadogo. Na hutumia kama kitoweo chake.
8- Black mamba anaishi katika mashimo ya miti na katika mashimo ya miamba. Pamoja na kiasi kikubwa cha sumu kali sana aliyonayo, lakini hana ujanja mbele ya Nguchiro na Mbweha, na Nyegere.
9- Black mamba hutembea haraka sana akiwa juu ya ardhi. Anaweza kusafiri umbali mrefu kwa kasi ya maili hadi 12 sawa na Kilomita 20 kwa saa. Hivyo usijaribu kukimbia atakufukuza mpaka akugonge sehemu ya mwili wako.
10- Jike hutaga mayai kati ya 10 na 25 katika kiota juu ya ardhi. Joto ni muhimu kwa ajili ya incubation ya mayai. Na mayai hujitotoa baada ya miezi 3. Na vijinyoka hivyo vichanga huanza kujihudumia kwa kila kitu na huwa na sumu ile ile kama ya nyoka mkongwe hivyo usije ukadharau.
11- Black mamba anaweza kuishi hadi miaka 11 katika pori na hadi miaka 12 katika kama atafugwa.
12. Nyoka huyu ana akili sana, anakula sana majani ya bangi, na mara nyingi hupenda kukaa kwenye mashamba ya bangi mida ya mc

Advertisements
%d bloggers like this: