Skip to content
Advertisements

Ice Boy atembelea nyota ya Darassa

Msanii Ice Boy amekanusha taarifa zinazosambazwa kuhusu yeye kutoka kimapenzi na mrembo ambaye anatajwa kuwa ni mpenzi wa rapa Darassa huku akidai kwamba hajawahi kufahamu kama wawili hao ni wapenzi na kujitetea kwamba yeye na binti huyo ni marafiki

Kupitia kipindi cha eNewz mapema wiki hii Ice Boy amefunguka na kusema kuwa mrembo huyo ni rafiki yake na wanafanya wote biashara na kila mmoja ana shughuli zake na vitu vingine kuhusu wao ni vya ndani zaidi, hivyo kukiri kwamba kilichoibua hilo ni baada ya kuweka picha kwenye mtandao wa instagram wakiwa pamoja.

“Kwa sababu tu nilimposti watu kibao wakachanganya mambo, sasa dili nini?, kwa sababu ni demu wa Darassa. Sio mvutano, sidhani kama ni mvutano kwa sababu mimi sijawahi kuonana naye au kupata comment kutoa kwake hata sijawahi kujua kwamba ni demu wake,” 

“Kama ni wanawake wapo tu na mimi nimeshakuwa kwenye mahusiano na warembo wengi tena watu maarufu kibao lakini sijawahi kuwaweka mtandaoni kwa sababu najua paparazi wapo lakini kwa huyu nimemuweka kama rafiki sina maana nyingine,”

Katika utetezi wake Ice Boy amedai kuwa yawezekana pia msanii Darassa ameshawahi kuwa na wanawake wengi ambao sasa hivi hana mpango nao hivyo kwake mrembo huyo hata akiamua kurudi kwa mpenzi wake yeye hana shida.

“Halafu you never know unaweza kukuta Darassa ameshawahi kudate na mademu kibao ambao wanadate na wana tu halafu yeye mwenye hana hata mchongo nao kwa sababu mademu siwapo tu mshikaji wangu,” amesema Ice Boy.

Advertisements
%d bloggers like this: