Skip to content
Advertisements

FAIZA ALLY: WASANII BONGO HAWANA UBUNIFU WA KUTAFUTA KIKI

IMEZOELEKA katika Muziki wa Bongo Fleva kwamba msanii akitaka kutoa wimbo mpya ni lazima kwanza afanye vituko mbalimbali ili watu wamzungumzie ndipo aachie ngoma yake. Mwanamitindo maarufu ambaye pia ni mfanyabiashara, Faiza Ally, amesema wasanii wa Tanzania hawana ubunifu katika katika kutafuta kiki.

Faiza ambaye amejifungua mtoto wa pili hivi karibuni, ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

“Nilichogundua sasa hivi kutokana na kipindi ninachosikilizaga redioni ni kwamba wasanii Watanzania hawana akili za ubunifu katika kutafuta kiki, zaidi ya wanaume kutoka na wanawake maarufu na wanawake maarufu zaidi ya kutoka na wanaume maarufu.

“Unapokuwa msanii kiki ni moja ya kazi lakini jaribu kuwa mbunifu kidogo zaidi ya uroda! Sema naomba mnisamehe ni ile uhuru wa kuongea tu sijamlenga mtu lakini najua kuna mstari wa kujifunza” ameandika Faiza.

Advertisements
%d bloggers like this: