Skip to content
Advertisements

FID Q ATUPA MOYO KUHUSU KITAALOJIA

Rapa Fareed Kubanda, FID Q amekuja tena nakutupa matumaini kuhusu ujio wa album yake, KITAALOJIA iliyosubiriwa kwa muda mrefu.

Akizungumza na Planet Bongo ya EA RADIO, Fid alisema,

“Naweza kusema itatoka mwaka huu, kilichokwamisha mpaka sasa ni ishu za Duplication. Muda ukifika itakuwa sokoni tu.”- alisema Fid na kuendelea

“KitaaLojia itakuwa ni album ya tofauti sana, kwanza kuanzia kwenye package. Pia kwa madini yaliyomo ndani, album hii inafaa kutumika hata kwenye Mitaala ya shule, kwa hiyo waisubiri.”- alimaliza rapa huyo ambaye amerudi masikioni mwetu kwa goma lake jipya, FRESH

Advertisements
%d bloggers like this: