Skip to content
Advertisements

Sare Za JWT Zamfikisha Mahakamani Mwingine Leo

Mfanyabiashara wa mmoja wa Kariakoo, Casto Ngogo (35) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kukutwa na suruali 5,000 za Jeshi la Wananchi (JWTZ), t-shirt na vitu.
Mshtakiwa huyo amesomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali, Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amedai kuwa Ngogo ambaye ni mkazi wa Tabata Segerea, June 15, 2017 alikutwa na vifaa vya JWTZ katika eneo ya Bandari kavu ya Galco Inland Container iliyopo Sokota Chang’ombe.
Wakili Simon amedai siku hiyo, mshtakiwa alikutwa na suruali 5,000 za JWTZ zenye thamani ya shilingi Milioni 50 pesa za Kitanzania ambazo zimepatikana kwa njia haramu.
Ngogo anadaiwa pia June 15, 2017 katika eneo hilo alikutwa na Maofisa wa Jeshi la Polisi akiwa na t-shirt 50 za JWTZ zenye thamani ya shilingi 500,000 pesa za kitanzania.
Mshtakiwa hakuruhusiwa kuongea chochote kwa sababu makosa yanayomkabili ni makosa ambayo mamlaka ya kuyasikiliza ni Mahakama Kuu.

Advertisements
%d bloggers like this: