Skip to content
Advertisements

Aliyekuwa mume wa Aunt Ezekiel adaiwa kuachiwa huru Dubai

DAR ES SALAAM: Aliyekuwa mume wa staa wa filamu Bongo Aunt Ezekiel, Sunday Demonte ambaye alikuwa akitumikia kifungo huko Dubai, anadaiwa kuachiwa na sasa yupo uraiani jijini Dar. 
Chanzo kimoja kilicho jirani na familia hiyo kililidokeza Risasi Mchanganyiko kuwa Demonte aliachiwa kutoka katika adhabu yake iliyotokana na kuishi kinyume cha sheria huko Dubai kwa muda sasa na kwamba yupo Dar. 
Baada ya kupata ubuyu huo, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta mdogo wa Demonte, ambaye ndiye alifunga ndoa na Aunt kwa niaba yake, aliyejitambulisha kwa jina la Shaban ambaye alikiri kaka yake kuwa huru. 

“Sunday mbona ameshatoka kitambo, yupo zake uraiani kwa raha zake, ni mwaka huuhuu ametoka japo sikumbuki ulikuwa mwezi wa ngapi maana sikuwepo, kwa sasa yupo hapa Dar, hayupo Dubai, ukitaka kujua mengi ni vizuri nikuunganishe naye mwenyewe ukamuhoji,” alisema. 
Hata hivyo, Shaban ambaye alisema atakuwa tayari kumuongoza mwandishi wetu kukutana na mume huyo wa ndoa wa Aunt, baadaye hakutoa tena ushirikiano. 

Kutokana na ishu hiyo shushushu wetu alizungumza na Aunt kujua kama ana taarifa hizo za mumewe kuwa uraiani, ambapo alidai hafahamu chochote kuhusu hilo kwani anavyojua yeye bado hajatoka gerezani.

Advertisements
%d bloggers like this: