Skip to content
Advertisements

MIAKA 20 JELA KWA KUWADHALILISHA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI.

TABORA: Mwanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma(TPSC), amehukumiwa miaka 20 jela kwa kuwadhalilisha Wanafunzi wa Shule ya Msingi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Emmanuel Ngigwana alitoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka wakiwamo wanafunzi waliodhalilishwa. .
Mshtakiwa huyo alikutwa akiwaonesha wanafunzi picha za ngono kupitia simu yake ya mkononi pia aliwashawishi wanafunzi hao wamshike sehemu za siri, huku na yeye akiwachezea. .
Baada ya kufanya upekuzi katika simu ya mshtakiwa, ilikutwa ikiwa na picha 197 za ngono na video 40 zikiwamo za watoto, watu wazima na wanyama.

Advertisements
%d bloggers like this: