Skip to content
Advertisements

Serikali yajibu Tundu Lissu

Serikali kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari, Zamaradi Kawawa imejibu hoja zilizotolewa na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kuhusu ununuzi wa ndege za Bombadier

Zamaradi Kawawa amekiri kuwa ni kweli ununuzi wa ndege hizo umeingiliwa na mgogoro ambao yeye anadai kuwa ni mgogoro wa kutengeneza na kusema umetengenezwa na wanasiasa wa Tanzania wasioitakia mema nchi ya Tanzania. 

“Ununuzi wa ndege ya 3 ya Bombadier umeingiliwa na mgogoro uliotengenezwa na wanasiasa na watu wasioitakia mema Tanzania, Wanasiasa waliotengeneza mgogoro huo wanahujumu maendeleo ya nchi na usalama wa raia”- alisema Zamaradi Kawawa

Aidha Zamaradi Kawawa amesema kuwa ndege ya tatu ambayo ilikuwa inatarajiwa kuingia nchini mwezi Julai amedai kuwa itaingia muda si mrefu na kuwataka Watanzania waiamini serikali ya Tanzania iliyopo chini ya Rais John Pombe Magufuli 

“Ndege ya 3 ya Bombadier ipo na inakuja kwahiyo wananchi waiamini Serikali yao ila serikali imesikitishwa na ushiriki wa wanasiasa na baadhi ya watu kuhujumu maendeleo ya nchi, Watanzania tuwe wazalendo kulinda, kutetea na kukabiliana na hujuma zozote zinazorudisha nyuma maendeleo ya Nchi, tuunge mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuleta maendeleo bila kujali itikadi ya chama, kabila au dini” alisisitiza Zamaradi Kawawa

Mbali na hilo Kawawa amesema kuwa serikali imeanza kuchukua hatua kadhaa kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hizo 

“Kuhusiana na mgogoro wa ununuzi wa ndege hatua za Kidiplomasia na sheria zimeanza kuchukuliwa ili kumaliza jambo hili” alisema Zamaradi Kawawa

Jana Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu alisema kuwa kutokana na maamuzi mbalimbali ikiwepo kuvunja kwa mikataba ya wawekezaji nchini imepelekea mali za Tanzania ikiwepo ndege aina ya Bombadier kushikiliwa nchini Cannada, na aliitaka serikali kusema ukweli juu ya jambo hilo kwa wananchi. 

Advertisements

1 Comment »

%d bloggers like this: