Skip to content
Advertisements

Chadema yathibitisha kukamatwa kwa Ester Bulaya

Moja ya taarifa zilizopo ni pamoja na hii ambayo kuhusu Mbunge wa Bunda Mjini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Ester Bulaya kukamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Rorya katika Mkoa wa Mara akiwa katika majukumu ya kichama.
Kukamatwa kwa Bulaya kumethibitishwa na Msemaji wa CHADEMA Tumaini Makene kuwa amekamatwa akiwa akiwa katika Hoteli aliyofikia Tarime ambako alikwenda kwa ajili ya shughuli za kichama.
Msemaji wa CHADEMA, Tumaini Makene: -”Ni kweli tumepata taarifa muda sio mrefu kwamba Mbunge wetu Jimbo la Bunda Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi akiwa Hotelini kwake, Tarime. Alikuwa katika shughuli za kichama akiwa kama Mbunge na Mjumbe wa Kamati Kuu.”

Advertisements
%d bloggers like this: