Skip to content
Advertisements

Mkuu wa Bunge la Burkina Faso ,Salif Diallo afariki dunia

Mwanasiasa na mkuu wa bunge la Burkina Faso ,Salif Diallo afariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili jijini Paris. 

Kwa mujibu wa habari,Salif Diallo mwenye umri wa miaka 60 amefariki katika hoteli aliyokuwa akikaa mjini humo. 
Ripoti zinaonyesha kuwa siku chache zilizopita bwana Diallo alifanyiwa upasuaji mjini Tunis. 
Salif Diallo amekuwa akiliongoza bunge la Burkina Faso toka mwaka 2015. 
Sababu kamili ya kifo chake haijajulikana.

Advertisements
%d bloggers like this: