Skip to content
Advertisements

Baada ya Serikali kumnyang’anya mashamba, Sumaye afunguka mazito

Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu wa Jamhiri ya Muungano wa Tanzania, Frederick Sumaye amesema kunyang’anywa mashamba yake si sababu ya yeye kufikiria kurudi CCM. 

“Kunyang’anywa mashamba yangu najua ni uamuzi wa juu haunidhoofishi nifikirie kurudi CCM’’ 

Sumaye amesema mashamba yaliyofutwa na Serikali yalikuwa yanalipiwa kodi na yalikuwa yanamilikiwa kisheria. 
“Wanataka nirudi CCM, mimi sitaki kurudi CCM, kwanini wananilazimisha? Nilisema sababu za kuondoka huko, waseme wazi sababu za kuyafuta ni za kisiasa tu,” amesema Sumaye leo katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Advertisements
%d bloggers like this: