Skip to content
Advertisements

Goodluck atekwa na Queen Fifi

Msanii wa muziki wa injili ambaye pia ni fundi kwenye uandishi wa mistari mikali kwenye game ya bongo fleva, Goodluck Gozbert au Loly Pop, amefunguka juu ya hisia zake kwa rapper wa kike bongo ambaye pia ni mtangazaji wa East Africa Radio Queen Fifi.

Akipiga stori na Big Chawa wa East Africa Radio, Goodluck amesema anampenda sana binti huyo tangu alipomuona kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya kusaka vipaji bongo, na kushindwa kujizuia juu yake.

Goodluck anafahamika kwa kuimba nyimbo za muziki wa injili aliendelea kusema kuwa Frida ni msanii ambaye alikuwa anamuangalia sana na akavutiwa naye, na kipaji chake ni cha aina ya kipekee, na hajawahi kuwa ‘bored’ anapokuwa naye.

Advertisements
%d bloggers like this: