Skip to content
Advertisements

ROSA REE: SIONI TATIZO KUJIACHIA NUSU UTUPU

M SANII anayekuja vizuri kwenye muziki wa Hip Hop, Rose Robert ‘Rosa Ree’ amefunguka kuwa hasumbuliwi na maneno ya watu wanaomzungumzia kuhusu mavazi yake ya nusu utupu kwani haoni tatizo lolote.

Akizungumza na Risasi Vibes, Rosa Ree alisema watu wanamhukumu wakati hawafahamu undani wa maisha yake ya nyuma (back ground) hivyo ni bora wanyamaze maana hawezi kuacha kuzivaa.

“Navaa mavazi ya nusu utupu kwa sababu napenda, mimi ni mwanamuziki, lazima nivae tofauti na watu wa kawaida, kwa hiyo wanataka hata nikienda kuoga nivae suruali? Acha waseme, ninaziba masikio mimi naangalia muziki wangu tu,” alisema.

Advertisements
%d bloggers like this: