Skip to content
Advertisements

Wizkid ni kitu kidogo kwangu” – Country Boy

Msanii wa muziki wa bongo fleva Country Boy, amesema kitendo cha mashabiki kumuita Wizkid wa bongo wako sahihi, kwani hata hivyo yeye ni zaidi ya Wizkid.Akizungumza na mwandishi wetu Country Boy amesema ubora wa kazi zake sasa unaenda kimataifa hivyo anaona ni sawa mashabiki wake kumbatiza jina hilo, na anakusudia kuwa zaidi ya msanii huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri mpaka Holywood.

“Nadhani nastahili zaidi ya hivyo kwa kila kitu sio tu Wizkid, Wizkid ni kitu kidogo sana kwenye taswira ya muziki wangu, natamani niwe mtu ukimzungumzia Country Boy, dunia nzima imjue ni nani”, alisema Country Boy.

Advertisements
%d bloggers like this: