Skip to content
Advertisements

P Funk Majani na Harmorapa wazinguana

Msanii wa hip hop bongo Harmorapa, amefunguka juu ya kitendo cha kumchana mtayarishaji wa muziki ambaye iliaminika anamkubali zaidi, na kukiri kuwa kwa sasa hayuko vizuri na P Funk. 

Akizingumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Harmorapa amesema kwa sasa hawana mawasiliano mazuri na P Funk, kwani kuna mambo ambayo yalitokea, yaliyosababisha kutoelewana kwao, 
“Nikimzungumzia Majani, kwenye maisha mtu unapitia sehemu nyingi, mfano mimi nafanya kazi kwa mtu halafu maslahi siyaoni, nafanya kazi kwa jasho najituma halafu yeye ndiyo ananufaika, halafu anakuona wewe humfai, na mwisho wa siku ndiyo inakuwa hivyo”, alisema Harmorapa. 
Harmorapa kwa sasa ameachia wimbo wake ambao umeonekana kumchana P Funk Majani ambaye alimsimamia kwenye kazi yake ya Nundu, na kumuunganisha na baadhi ya watu ili aweze kufanikisha kazi zake za muziki.

Advertisements
%d bloggers like this: