Skip to content
Advertisements

Hamilton ampa somo Sebastian Vettel michuano ya Belgian Grand Prix

Dereva wa magari ya Mercedes Mwingereza, Lewis Hamilton ameibuka mshindi wa mbio za Belgian Grand Prix akimshinda mpinzani wake mkubwa wa timu ya Ferrari, Sebastian Vettel.

Hamilton mwenye umri wa miaka 32, alitumia muda wa saa moja, dakika 24 na sekunde 42 nakutosha kumpatia ubingwa huo akiwazidi wapinzani wake alama 25.
Mpinzani wake dereva wa Ferrari, Sebastian Vettel alishika nafasi ya pili katika mashindano hayo kwa kupata alama 18 huku Daniel Ricciardo, toka timu ya Red Bull, akimaliza katika nafasi ya tatu kwa kupata alama 15.
Baada ya ushindi huo, Hamilton amesema “Nilikuwa nahitaji kushinda haya mashindano. Nilivyokuja hapa niliwaambia sababu ya mimi kuja kwaajili gani na siwezi kuondoka bila ya hiko kitu na hatimaye nimefanikiwa kupata nilicho kikusudia”

Advertisements
%d bloggers like this: