Skip to content
Advertisements

ZAMARADI MKETEMA: MUZIKI KWA SASA UPO KWA ASLAY TU

WASWAHILI wanasema mapenzi ni kikohozi na kuyaficha huwezi. Msemo huu umedhihirika kwa mtangazaji wa kituo cha televisheni, Zamaradi Mketema, ambaye ameweka wazi mapenzi aliyo nayo na anavyomkubali msanii, Aslay, kimuziki.

Zamaradi ameonyesha wazi kumkubali zaidi Aslay, anayetamba na ngoma zake kama Likizo, Baby, Pusha na nyingine nyingi, kuliko msanii yeyote yule, na kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka mambo hadharani.

Zamaradi Mketema,


“Tukiacha utimu ambao hauna ubaya labda ndiyo unafanya kuwe na uhai wa muziki na kupatikane vitu vya kuongelea, ila muziki kwa sasa upo kwa Aslay.
“Natamani Watanzania wangemwelewa katika hali ya ukubwa aliyo nayo, najua wanamtambua ila natamani tu wangemtambua zaidi; huyu mtoto ni habari nyingine,” ameandika Zamaradi.

Advertisements
%d bloggers like this: