Skip to content
Advertisements

AMANDA AJINADI KUWAZIDI SHILOLE NA SNURA

Msanii Mwenye mvuto wa kipekee kwenye tasnia ya filamu Tamrina Poshi maarufu Amanda amesema kuwa katika maisha yake alikuwa anapenda kuimba sana mduara na anamini anauwezo wakuutendea haki.
Akizungumza na DigitalDrimz Amanda amesema alitamani kuwa msanii wa mduara lakini uigizaji ndiyo ulichukua nafasi kubwa kwake huku akiamini kuwa atawafunika wasanii mwenye majina makubwa kwenye aina hiyo ya muziki.


“Nilikuwa na ndoto yakuwa mwanamuziki hasa wa mduara mana ndio muziki ninaoupenda lakini badala yake uigizaji umeweza kuchukua nafasi kubwa na kuonekana kama naegemea upande mmoja na hiyo ni kwa sababu sikupata mtu wakunisimamia kwenye muziki ila kwa sasa naanza kujisimamia mwenyewe na naamini nitawapoteza kabisa hata wakina Snura na Shilole” alisema Amanda.

Advertisements
%d bloggers like this: