Skip to content
Advertisements

Lady Jay Dee: Wabongo Wanashobokea Sana Wa Nje

Lady Jay Dee amesema wabongo wanapenda sana kushobokea wasanii wa nje kuliko wale walionao ndani, Jay Dee ametoa kauli hiyo kupitia kipindi cha The Finest kinachorushwa na Redio 92.9 A. FM yenye maskani yake mjini Dodoma. 

Lady Jay Dee alisema, Madj na Mapresenter wa Tanzania, wanapiga sana nyimbo za nje kuliko za bongo, na pia Wasanii wa Tanzania wamekuwa wanafuata upepo ulipo katika kazi zao, ukija mtindo wa Nigeria wanaimba kama nigeria, ikija ya south wanaimba kama wao, hivyo bongo flava haijui identity yake ni ipi. 
Lady Jay Dee amesema hataki mazoea na watu asiowajua na ndio mana watu wengi wamekuwa wakisema kuwa anaringa ila si kweli. 
Jay Dee ameongeza kuwa yeye sio muongeaji na huwa ni vigumu sana kwake kupiga mastory na mtu ambaye hajamzoea, japo salamu anatoa. 
Hata hivyo kwa mara nyingine tena mwanadada huyu atafanya vitu vyake akiwa na mpenzi wake Spicy and the band Siku ya leo Eid mosi ndani ya kiota kipya cha Burudani Dodoma Capetown , akisindikizwa na mkali wa singeli Msaga Sumu na Nay wa Mitego. 

Advertisements
%d bloggers like this: