Skip to content
Advertisements

SIAMINI KAMA ALIKIBA NA DIAMOND WAMETUZIBIA NAFASI WASANII WENGINE – LULUDIVA.

Amezungumza Mrembo Lulu Diva Ambaye Kwa Sasa Anafanya Poa Na Ngoma Yake Mpya Iitwayo Give It To Me Ngoma Ambayo Imekuja Na Majibu Mengi Na Maswali Huku Katika Video Moja Ya Kipande Kilichozua Maswali Ni Alipokuwa Akiimba Ndani Ya Maji Na Kukiri Kuwa Ni Moja Ya Kipande Kilichompa Wakati Mgumu Sana Lakini Ilikuwa Njia Ya Kuleta Utofauti Katika Video Hiyo Jambo Ambalo Kweli Limeonyesha Utofauti Hali Ya Kuwa Alipata Uoga Sana Wakati Wa Utengenezaji Wa Video Hiyo.
Kufutia Yote Yuanayoendelea Katika Mitandao Ya Kijamii Kwasasa Inaonekana Asilimia Kubwa Wanaotrend Ni Alikiba Pamoja Na Diamond Jambo Ambalo Nyuma Kuna Wasanii Wengi Wametoa Kazi Zao.
Sasa Digital Drimz Ilitaka Kujua Kwa Upande Wa Lulu Diva Kufuatia Kinachoendelea Je,Imemzibia Nafasi Ya Muziki Wake Kama Mtaa Unavyosema,Na Lulu Diva Alitujibu Kama Ifuatavyo:-

“Mimi Binafsi Sioni Kama Kuna Kitu Cha Namna Hiyo Mimi Naamini Katika Mziki Mzuri N Ahata Ukiangalia Ngoma Yangu Tangu Nimeiachia Inafanya Vizuri Kwa Hiyo Mziki Mzuri Ndio Unanguvu Kubwa Zaidi Kuliko Kitu Kingine “

Alisema Lulu Diva Ambaye Alizidi Kusisitiza Kuwa Kuna Makubwa Yanakuja Kati Yake Na Ana Jambo Kati Yake Na Beyonce Ambaye Ni Moja Kati Ya Wasanii Anaowapenda Sana So Lolote Laweza Kutokea.

Advertisements
%d bloggers like this: