Skip to content
Advertisements

Viongozi watano Boko Haram wauawa

Jeshi la Nigeria limetangaza kwamba, limewauwa makamanda watano wa ngazi ya juu wa kundi la Boko Haram, wakati jeshi hilo likiongeza mashambulizi dhidi ya kundi hilo katika eneo Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. 

Msemaji wa Jeshi Sani Usman, amesema, idadi kubwa ya wapiganaji wa Boko Haram pamoja na viongozi wao waliuwawa katika shambulizi la mabomu lililotekelezwa na ndegevita za serikali. 
Kundi la Boko Haram limeuwa watu zaidi ya elfu 20 na kusababisha wengine milioni 2.3 kuyakimbia makazi yao tangu lilipoanzisha mashambulizi mwaka 2009.

Advertisements
%d bloggers like this: