Skip to content
Advertisements

BWENI LA WASICHANA LATEKETEA KWA MOTO, SABA WAFARIKI DUNIA!

Watoto waliozirai wakisaidiwa na Kikosi cha Msalaba Mwekundu.

Bweni la Shule ya Wasichana ya Moi iliyopo Kibera jijini Nairobi, limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya wanafunzi saba huku wengine 10 wakijeruhiwa.

Wazazi wakiwachukua watoto wao.

Waziri wa Elimu nchini humo, Fred Matiang’i amethibitisha kutokea kwa tukio hilo la kuhudhunisha huku akieleza kuwa vifo na majeraha mengi yametokana na kukanyagana baada ya taharuki na wengine kuruka kupitia madirishani ambapo majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa Hospitali ya Wanawake ya Nairobi kutibiwa.

Waziri wa Elimu nchini humo, Fred

Matiang’iakiwatuliza wanafunzi na walimu wa shule hiyo.

Matiang’i ameifunga shule hiyo kwa wiki mbili kutokana na ajali hiyo na kuwataka wazazi wawachukue watoto wao wakati uchunguzi wa moto huo ukiendelea. Ameeleza kuwa wanafunzi wa kidato cha nne watarudi shuleni hapo Ijumaa ijayo kwa ajiri ya maandalizi ya mtihani wa kuhitimu elimu ya sekondari.

Advertisements
%d bloggers like this: