Skip to content
Advertisements

DAR: ALMASI YA BILIONI 32.8 YANASWA AIRPORT IKIPELEKWA UBELGIJI

JESHI la Polisi limekamata almasi yenye uzito wa kilo 19.5 inayokadiriwa kuwa na thamani ya Sh. bilioni 32.8 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, Martine Otieno amesema madini hayo yalikuwa yakitolewa kwenye Mgodi wa Mwadui yakisafirishwa kwenda nchini Ubeligiji.

Inadaiwa waliohusika ni kampuni moja ya Afrika Kusini. Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Merdald Kalemani atazungumza na waandishi wa habari kufafanua tukio hilo.

Advertisements
%d bloggers like this: