Skip to content
Advertisements

Moto mkubwa wateketeza maeneo ya Los Angeles, Marekani

Moto ukionekana kutoka katikati ya mji wa Burbank

Mamia ya wakazi wa jiji la Los Angeles, katika jimbo la Califronia wameruhusiwa kurejea makwao, baada ya moto mkubwa wa nyikani ambao ulikuwa umeathiri eneo kubwa kuanza kuthibitiwa.

Moto huo ulikuwa umeathiri eneo la ukubwa wa eka 5,000 na ulianza katika hori ya La Tuna Canyon siku ya Ijumaa.

Kuzuka kwa moto huo kulisababisha kutangazwa kwa hali ya dharura.

“Tumepiga hatua kubwa, lakini bado haujadhibitiwa kabisa,” Meya Eric Garcetti amesema, na akaonya kwamba hali huenda ikabadilika kutokana na kuwepo kwa upepo mkali.

Mamia ya watu walihamishwa kutoka nyumba zao Burbank, California

Nyumba tatu ziliteketezwa na moto huo na inaarifiwa watu wanne wamejeruhiwa.

Moto huo ndio mkubwa zaidi kuwahi kuzuka katika historia katika eneo hilo.

Wakazi walikuwa wamehamishwa kutoka maeneo ya Glendale na Burbank lakini wakaruhusiwa kurejea baada ya mvua iliyokuwa ikinyesha bado na kuwepo kwa hewa baridi kuwasiadia wazima moto kuudhibiti.

Ndege zilitumiwa kumwaga kemikali na maji kulinda nyumba karibu na Burbank

Majimbo mengine nchini Marekani, maeneo ya magharibi, yamekuwa wakitatizwa na mikasa ya moto.

Tayari serikali za majimbo ya Montana na washington zimetangaza dharura na wakazi katika baadhi ya maeneo wamehamishwa.

Moto huo wa La Tuna tayari umeteketeza eka 5,000

Advertisements
%d bloggers like this: