Skip to content
Advertisements

WEMA ALAMBA DILI LA MIL. 400

DAR ES SALAAM: Staa mkali wa sinema za Kibongo asiyechuja Bongo, Wema Isaac Sepetu, anadaiwa kulamba dili nono la shilingi milioni 400 kutoka kwenye kampuni moja kubwa ya ving’amuzi Afrika yenye makao yake makuu nchini Afrika Kusini.
 

Habari kutoka kwenye chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa staa huyo zilieleza kuwa, dili hilo alilopata Wema ni kwa ajili ya kutengeneza tamthilia na sinema kupitia kampuni yake ya Endless Fame ambazo zitaruka kwenye kituo hicho na kuambulia donge hilo nono.

“Wema sasa hivi atakuwa mtu mwingine kabisa kwa sababu dili hilo akikabidhiwa kabisa atarejea kwenye ile status yake ya kuitwa pedeshee mwanamke na hata marafiki waliokuwa wameyeyuka watarudi,” kilinyetisha chanzo hicho.

Mpashaji huyo aliendelea kufunguka kuwa, Wema anatarajia kuwakusanya kampani yake yote ya Endless Fame kwa ajili ya tenda hiyo ambayo itakuwa ni ya aina yake.

 

Baada ya kudaka habari hizo njema kuhusu Wema ambaye wengine humuita ‘Keki ya Taifa’ au ‘Tanzania Sweetheart’, Ijumaa Wikienda lilimsaka lakini halikufanikiwa badala yake lilimpata mmoja wa waratibu wa kazi zake ambaye alikiri kuwepo kwa dili hilo, lakini bado halijakamilika mpaka leo (Jumatatu).

 

“Duh! Ninyi noma, mmeinyaka? Ni kweli hilo dili lipo, lakini nafikiri litakamilika Jumatatu ijayo (leo),” alinyetisha mdau huyo.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, simu ya Wema ilikuwa ikiita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa SMS hakuwa amejibu.

Advertisements

1 Comment »

%d bloggers like this: