Skip to content
Advertisements

Chid Benz aanza kuwajibu

Msanii Chid Benz anaonekana kuendelea kupambana na watu wanaomtuhumu kuwa amerukwa na akili kwa matumizi ya madawa ya kulevya, ambapo leo amemtolea povu Dj Choka na kusema hana hadhi ya kumjadili kwani kwake ni mtoto mdogo.

Akiongea kwenye eNewz inayorushwa na East Africa Television, Chid Benz amesema Dj Choka ni mtu ambaye amekuwa huku anamuona, hivyo anatakiwa amuheshimu kwani yeye ni mkubwa kwake.

“Dj Choka ni mdogo wangu, ni mtoto ambaye anakua tunamuona tunamfundisha vitu viwili vitatu, hajakosea sana ila tu amejaribu kufanya vitu ambavyo labda yeye kuna watu wamemtengeneza afanye kwa manufaa ya hao watu na kwa manufaa ya kwake, sasa nisimpe nafasi kubwa sana sababu yeye anajijua kwamba mimi ni mkubwa kwake, na yeye asitengeneze picha yoyote tofauti atakuwa ananivunjia heshima”, alisema Chid Benz.

Hivi karibuni Dj Choka baada ya kuona video ya Chid Benz kusema amefanya video na Tupac, alipost video ya mtoto akiwa anacheka kwenye Instagram, kitendo kinacho onekana kilimkera Chid benz na kuamua kumfuata ‘inbox’ kumwambia aitoe.

Advertisements
%d bloggers like this: