Skip to content
Advertisements

Polisi wamshikilia mwanasiasa wa Upinzani

Diane Rwigara

Polisi nchini Rwanda wamesema wanamshikilia mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara, mama yake pamoja na dada yake.

Wiki iliyopita polisi walikuwa wametangaza kuwa mwanasiasa huyo anatuhumiwa kughushi nyaraka wakati alipotaka kuwania urais mapema mwezi uliopita huku familia yake ikituhumiwa kukwepa kulipa kodi.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, polisi wapatao 10 wameingia kwenye makazi anapoishi mwanasiasa huyo na familia yake mtaa wa Kiyovu mjini Kigali na kuruka juu ya lango baada ya kukataliwa kufunguliwa na kumkamata mwanasiasa huyo pamoja na Mama yake na dada yake.

Duru za polisi zimesema kwamba polisi wameamua kwenda kuwakamata baada ya wao kushindwa kuripoti katika idara ya upelelezi ya polisi mara kadhaa.

Wiki iliyopita, polisi wa Rwanda walitangaza kufanya upekuzi katika makazi ya mwanasiasa huyo na kutangaza kwamba ni sehemu ya upelelezi wa mwanzo kuhusu tuhuma za kughushi nyaraka na kukwepa kulipa kodi. Diane Rwigara alikataliwa kugombea kiti cha urais katika uchaguzi uliofanyika mwezi wa 8 na baada ye akaanzisha vuguguvu la kukosoa utawala wa nchi hiyo.

Advertisements
%d bloggers like this: