Skip to content
Advertisements

LESOTHO:KAMANDA WA JESHI , LUTENI JENERALI KHOANTLE MOTSOMOTSO AMEUWAWA KWA KUPIGWA RISASI

Kamanda wa Jeshi nchini Lesotho, Luteni Jenerali Khoantle Motsomotso ameuwawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wenzake, kwa mujibu wa maafisa kutoka nchini humo.
Waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Sentje Lebona amethibitisha kifo hicho cha Luteni Jenerali Khoantle Motsomotso siku ya jumanne asubuhi.
Aliuwawa akiwa nyumbani kwake na kundi la wanajeshi ambao walikuwa wamefukuzwa kazi siku si nyingi, alisema Ramanka Mokaloba, Afisa wa ulizi, kwa mujibu wa wakala wa habari DPA.
Mwanajeshi mmoja aliuwawa wakati wa vamizi hilo na mwingine kujeruhiwa.
Lesotho imekuwa ikikabiliwa na mapambano ya nguvu kuhusiana na jeshi kuingilia siasa za nchi hiyo. Nchi hiyo imekumbwa na matukio kadhaa ya mauaji ya watu wakubwa, kujumuisha na mauwaji ya Mkuu wa Jeshi mwaka 2015.

Advertisements
%d bloggers like this: