Skip to content
Advertisements

VIDOKEZO VYA MAGAZETI

Kamati iliyochunguza biashara ya Almasi jana ilisema kuna kiongozi mmoja alipewa zawadi Almasi yenye thamani ya Tsh 448.4 bilioni (USD 200m) 

Mbunge Hussein Bashe asema muda wa kubadili katiba na kuondoka kinga kwa Marais umefika kwani ndiyo huwafanya kufumbia macho baadhi ya vitu. 

CHADEMA wasema Bunge limevunja sheria kuomba fedha za ziada nje ya bajeti iliyoidhinishwa bila kupitisha maombi bungeni- MTANZANIA 

Mbunge wa K’ndoni, Maulid Mtulia asema hakuungana na wenzake wa UKAWA kutoka bungeni kususia kiapo cha wabunge wapya kwani hakutabadili kitu.

Chanzo ajali iliyosababisha vifo vya wanachama watatu wa CUF ni dereva kuyumba baada ya kupigwa mwanga mkali wa taa za lori- Nipashe.

Advertisements
%d bloggers like this: