Skip to content
Advertisements

SABBY AJITOSA KUPIMA ‘NGOMA’

MSANII wa filamu Bongo Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ameamua kujitosa kupima Ukimwi ‘ngoma’ ili kuwa na amani ya moyo na kusema kuwa wasanii wengi hawapendi kupima kwa kuhofia kona wanazopita huenda hawako salama.

Akipiga stori na Star Mix, Sabby alisema aliona ni bora akapime ili kujua usalama wa afya yake kuliko kukaa na wasiwasi kutokana na watu ambao amewahi kujihusisha nao kimapenzi.

“Nimefurahi baada ya kupima na kugundua niko poa, niwasihi wasanii wenzangu wakapime kujua afya zao, kuliko mtu unaishi tu bila kujijua kama una maambukizi au la,” alisema.

Advertisements
%d bloggers like this: