Skip to content
Advertisements

BURUDANIZ Anto aachia wimbo maalumu wa kumuombee afya njema Lissu

Msanii mkongwe wa Muziki, Z Anto ameingia studio na kurekodi wimbo maalumu kwaajili ya kumuombea afya njema Mbunge wa Singida kupitia tiketi ya Chadema, Tundu Lissu aliyelazwa nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake Area D, Dodoma muda mchache akitokea Bungeni.amesema amefanya wimbo huo maalumu ili kuwahimiza watanzania kuendelea kumuombea mwanasiasa huyo mpaka pale afya yake itakapo kuwa fiti.
“Dua ndio kila kitu kwa sasa, watanzania wote kwa dini zetu, tuungane kumuombea afya njema ndugu yetu kwa sababu tukio lililomkuta sio la kawaida kabisa katika maisha yetu ya kawaida,” alisema Z Anto.
Muimbaji huyo amedai alikuwa na mpango wa kuachia wimbo wake mpya wiki hii lakini amesitisha mpango huo na kuamua kuandaa wimbo maalumu ambao utawafanya watanzania kuombea afya njema Lissu.

Advertisements
%d bloggers like this: