Skip to content
Advertisements

JULIANA KANYOMOZI NA MSANII MWENZAKE DESIRE LUZINDA WALIAMSHA DUDE

Hii Ilitokea Mapema Wiki Hii Baada Ya Story Kusambaa Na Kudai Kuwa Mwanamama Juliana Anamnyemelea Mfanya Biashara Maarufu Lwasa Emmanuel Ambaye Ni Mchumba Wa Msanii Desire Luzinda.
Tuhuma Hizo Zilianza Kuzagaa Baada Ya Picha Ambayo Ilisambaa Kwenye Mitandao Ya Kijamii Juliana Kanyomozi Na Jamaa Huyo Wakiwa Pamoja Kwenye Ndege Kuelekea Marekani.
Lakini Kwa Mujibu Wa Juliana Kanyomozi Picha Hiyo Ilipigwa Pasipo Yeye Kuwa Makini Ama Kuwa Tayari Kwa Picha Na Kuamua Kufunguka Kupitia Mitandao Ya Kijamii Baada Ya Maneno Kuwa Mengi Zaidi.


“Huwezi Kuja Ukapiga Picha Na Mtu Kwa Sababu Imetokea Umekaa Naye Siti Moja Na yeye Kwenye Ndege Bila Ridhaa Yake Na Ukaenda Kuiweka Katika Mitandao Ya Kijamii Jambo Linaloonyesha Nasafiri Na Wewe,Hata Hukuwa Na Ukarimu Wa Kunisalimia Na uombe Picha Na Mimi Hii Inasumbua Maisha Binafsi Ya Watu Nitakushitaki “


Aliandika Juliana Kanyomozi Kupitia Mitandao Yake Ya Kijamii Ikiwemo Facebook Na Ndipo Kufatia Hatua Hiyo Desire Naye Hakuona Shida Sana Kuliamsha Kwa Upande Wake Mkali Huyo Wa Ekitone Aliamua Kufunguka Haya Kupitia Instagram Yake.

Desire Luzinda

“Wakati Mwingine Tunaibukia Vitu Visivyo Na Maana Wakati Katika Maisha Halisi Tuna Mapambano Ya Maumivu Na Msongo Wa Vitu Ndani Yetu Lakini Kama UkisaLi Kwa Nguvu Zake Yeye Pekee Atakuponya Kidonda Cha Moyo Uliovunjika,Na Ndipo Utaanza Kugundua Vitu Vidogo Ulivyokuwa Unavitilia Maanani Hata Havina Faida Kwako Na Hisia Zako”

Sasa Kufuatia kauli Hiyo Ya Desire Imeonekana Dhahiri Kabisa Msanii Huyo Amempa Dongo Bibie Juliana Kanyomozi Ambaye Kwa Sasa Anafanya Vizuri Na Wimbo Wake Uitwao Woman.
Lakini Kulingana Na Jibu La Juliana Ina Maanisha Dhahiri Hana Mahusiano Na Jamaa Huyo Kama Watu Walivyodhani.

Advertisements
%d bloggers like this: