Skip to content
Advertisements

Mke wa zamani wa Jacob Zuma achaguliwa kuwa mbunge Afrika Kusini

Mke wa zamani wa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amechaguliwa kama mbunge mpya wa bunge la nchi hiyo.
Wataalamu wanaamini kuchaguliwa kwa Nkosazana Dlamini-Zuma ni moja ya kampeni ya kumfanya kuwa kiongozi wa chama cha ANC(African Ruling Party).
Chama cha ANC ambacho kimeitawala Afrika Kusini toka mwaka 1994 kinatarajia kumchagua kiongozi wake mpya mnamo mwezi Desemba.
Kwa mujibu wa habari Nkosazana Dlamini-Zuma mwenye umri wa miaka 67 anatarajia kuapichwa wiki ijayo.
Ripoti zinaonyesha kuwa atakaeshinda kuwa kiongozi mpya wa ANC ana uwezo mkubwa wa kuwa rais mpya wa Afrika Kusini kwani chama hicho kina wafuasi wengi nchini humo.

Advertisements
%d bloggers like this: