Skip to content
Advertisements

PRODYUZA ZEST AFUNGUKIA MAAJABU YA ASLAY

MWIMBAJI wa Nyimbo za Injili ambaye pia ni prodyuza wa nyimbo za msanii, Aslay Isihaka, Zest Daud, ameshangazwa na maajabu ya Aslay anapokuwa kwenye biti.

Zest ambaye amefanya nyimbo nyingi za msanii huyo zikiwemo Muhudumu na Pusha, amekutana na Uwazi Showbiz na kufunguka mambo mengi yakiwemo uwezo wa kutunga na kuimba wa Aslay.

SHOWBIZ: Jina lako kamili ni nani, na umeanza u-prodyuza mwaka gani?

SHOWBIZ: Naitwa Zest Daud, u-prodyuza nimeanza mwaka 2012.

SHOWBIZ: Moja Moja ni nini?

ZEST: Ni studio ambayo iko ndani ya Moja Moja Empire, ina jumla ya wasanii watatu ambao ni Trible, Tatii, Y- Tony, kwa upande wa watayarishaji ni wawili, Erick na Ruge Touch.

SHOWBIZ: Kwa nini unasema Aslay ni msanii wa ajabu

ZEST: Hajawahi kuandika wimbo tangu nimeanza kufanya naye kazi.

SHOWBIZ: Unamaanisha haandiki au anafanyaje kazi zake za utunzi?

ZEST: Aslay bhana! Huwa anakuja na aidia yake, nikimtengenezea biti basi anavaa headphones na kuanza kutiririka. Hajawahi kuomba kalamu wala karatasi kwa ajili ya kuandika.

SHOWBIZ: Ilikuaje mkaanza kufanya naye kazi?

ZEST: Nimefahamiana naye kitambo sana hata kabla hajaingia Yamoto Band na nilimtengenezea Wimbo wa Kasema ambao haukufanya vizuri. Hata hivyo tunaheshimiana, ana kipaji, anajua kuimba, mimi pia nina kipaji cha kuprodyuzi.

SHOWBIZ: Ni nyimbo ngapi ambazo umemtengenezea hadi sasa?

REST: Ni nyingi sana zipo zilizotoka na ambazo bado hazijakamilika.

SHOWBIZ: Unaweza kututajia zilizotoka?

ZEST: Kidawa, Tete, Hautegeki, Koko, Usiitie Doa, Muhudumu, Pusha na Nyakunyaku ambayo ameiachia hivi karibuni.

SHOWBIZ: Anakulipa au mnafanyaje kazi zenu?

ZEST: Tuna makubaliano yetu sisi wenyewe ambayo si vyema kuyaanika wazi.

SHOWBIZ: Kwa hiyo wewe mwenyewe ndiyo meneja wake?

ZEST: Hapana, Aslay ana meneja wake anaitwa Chambuso ila mimi nahusika zaidi kwenye audio.

SHOWBIZ: Aslay ni mtu wa aina gani anapokuwa kwenye biti?

ZEST: Jamaa mkali sana, hajawahi kunisumbua kwa sababu ni mwanamuziki wa kweli.Yuko poa sana, anaweza kuishi na mtu yeyote, anashirikiana na kila mtu.

SHOWBIZ: Ukiachana na kuprodyuzi, unafanya ishu gani zingine?

ZEST: Mimi pia ni Muimbaji wa Muziki wa Injili, kwa sasa nina albamu yangu ya Nipokee ikiwa na nyimbo kama Best Friend Forever ‘BFF’, Watu wa Mungu, Chuki, Nibaki Nawe, Toa na nyingineo.

SHOWBIZ: Kuna wasanii gani wengine ambao umewahi kufanya nao kazi?

ZEST: Kuna wimbo wa Kala Jeremiah wa Wanandoto, Usikate Tamaa akiwa na Nuruelly, Nchi ya Ahadi kaimba na R.O.M.A, Malkia na Naylee, Y. Tony wa Kivuli, Kibenten na wasanii wengine wengi ambao kazi zao bado hazijatoka.

SHOWBIZ: Baada ya kutengeneza nyimbo za Aslay, mapokeo yamekuwaje?

ZEST: Nakushukuru Mungu ni makubwa kwani nimeongeza mashabiki na wasanii ambao wanataka kufanya kazi na mimi.

Advertisements
%d bloggers like this: