Skip to content
Advertisements

KAJALA, WOLPER KIMEWAKA MBAYA

DAR ES SALAAM: Kinachoendelea hivi sasa kati ya mastaa wawili wakubwa wa filamu, Kajala Masanja na Jacqueline Wolper tunaweza kusema kimewaka mbaya baada ya mazungumzo kwa njia ya video kati ya muigizaji huyo na aliyekuwa bwana wa mwenzake kuwekwa mtandaoni na kuibua makubwa.

Kajala alikuwa akizungumza kwa njia hiyo ya kisasa na msanii Rajab Abdulhan ‘Harmonize’, akionekana akila tunda aina ya ‘apple’ kitandani kwake, huku msanii huyo naye akiwa kitandani kwake, kabla ya kijana huyo mwenyeji wa Mtwara, kuirusha picha hiyo mitandaoni na kusababisha ubuyu kusambaa. Kitendo hicho kilionekana kumkera Wolper ambaye ndiyo kwanza ametoka kuachana na Harmonize, hivyo kushindwa kujizuia na kuandika chini ya picha hiyo maneno yafuatayo;

“Yaani nimekaa hapa mwenyewe nimewaza mapenzi ya siku hizi yana drama mno, mara leo huyo, mara kesho yule.” Akijua wazi muigizaji mwenzake ameumizwa na kitendo hicho, staa mwingine, Wema Sepetu aliingilia kati ishu hiyo na yeye kuandika kitu chini ya picha hiyo; “Be carefully my Edit

 huyo nyakunyaku asije akapita maana kaambiwa mlango uko wazi.


Maneno hayo yalionekana kumuuma Kajala, ambaye mara moja alikimbilia Kituo cha Polisi Mabatini, kwenda kumshtaki Harmonize kwa kitendo chake cha kuiweka picha hiyo mitandaoni na kuleta tafsiri kuwa huenda wawili hao ni wapenzi, kitu ambacho siyo cha kweli na yeye amepewa RB No KJN/ PE/73/2017 Jalada la uchunguzi.

“Harmonize nimemshitaki ili ajue mimi siyo mtu wa kuchezewa kila wakati, maana ile video tulikuwa tukizungumza kawaida, kwa nini aisambaze, ili iweje kama siyo kuchafuana huko,” alisema Kajala. Staa huyo aliongeza kuwa anawashangaa wasanii wenzake Wolper na Wema kuingilia vitu kama hivyo kwa sababu labda wanaona kama yeye ni wa kula mizoga yao.

“Mimi nashangaa sana, hivi wamenionaje, wanafikiri mimi ni wa kula mizoga yao nini wanayoiacha, wamenishangaza sana,” alisema Kajala Katika Kituo cha Polisi Mabatini, Risasi Mchanganyiko lilimshuhudia Harmonize akiwasili kusikiliza shauri hilo ambapo kwa mujibu wa habari za uhakika kituoni hapo, mwimbaji huyo alijitetea kuwa aliyeweka picha hizo mtandaoni alikuwa ni mwanamke wake wa Kizungu, ambaye alimtumia mtu mwingine akitaka kumjua kwa jina muigizaji huyo. Wema na Wolper hawakuweza kupatikana kuzungumzia ishu hiyo.

Advertisements
%d bloggers like this: