Skip to content
Advertisements

Upinzani Burundi watolea wito Umoja wa Mataifa kuwalindia usalama

Upinzani nchini Burundi watolea wito Umoja wa Mataifa kuwalindia usalama
Kambi ya wakimbizi Kamanyola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kunapatika wakimbizi 2 000 kutoka Burundi.
Muungano wa wapinzani nchini Burundi umetolea wito Umoja wa Mataifa Jumanne kuwalindia usalama wakimbizi wanaopatikana katika nchi jirani.
Muungano wa CNARED nchini Burundi umetuma barua kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ikiwa na ujumbe kuwa tangu Aprli mwaka 2015 watu zaidi 500 000 walilazimika kuondoka katika taifa lao baada ya kuzuka ghasia zilizosababishwa kwa mujibu wa upinzani na chama tawala kumteua rais Nkurunziza kuwania kiti cha urais kwa muhula wa tatu.
Kwa mujibu wa upinzani, askar iwa upelelezi wamejipenyeza katika kambi tofauti za wakimbizi na kuwatisha kurejea nchini Burundi.

Advertisements
%d bloggers like this: