Skip to content
Advertisements

Diego Costa apata timu mpya

Baada ya tetesi na mvutano wa muda mrefu kati ya Chelsea na Diego Costa hatimaye mshambuliaji huyo anahamia Athletico Madrid baada ya klabu hiyo kukubaliana na Chelsea. 

Taarifa zinasema ndani ya masaa 24 kuanzia sasa mshambuliaji huyo anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na anaweza kutangazwa kama mchezaji wa klabu hiyo kesho ama keshokutwa. 
Diego aligoma kabisa kurudi katika klabu ya Chelsea, klabu hiyo ililiweka jina lake katika majina ya wachezaji watakaoitumikia katika Premier League lakini wakamtosa katika kikosi cha Champions League. 
Duego Costa tangu mapema wakati wa dirisha la usajili aliweka wazi kwamba hataki kurudi darajani kutoka na uhusiano mbovu baina yake na kocha wa Chelsea na akaonesha matamanio yake kurudi Athletico Madrid. 
Lakini Athletico Madrid hawataweza kumtumia Diego Costa kwa sasa kwani wanatumikia kifungo cha usajili hivyo itamlazimu Costa kusubiri hadi January kuvaa jezi ya Athletico Madrid kwa mara nyingine. 
Chelsea walimnunua Diego Costa kutoka Athletico Madrid mwaka 2014 kwa ada ya £32m na sasa wanamuuza kwa ada ya £53m kurudi tena katika klabu yake hiyo ya zamani. 
Mapema mwezi hui ilionekana kama Costa anaweza kubaki Chelsea baada ya kuonekana Uingereza na huku golikipa wa Chelsea akitweet picha ambayo ilikuwa na caption inayoonesha Costa anabaki. 
Diego Costa tangu ajiunge Chelsea amewafungia jumla ya mabao 52 katika michezo 89 huku akichangia kutoa assist 16 na msimu uliopita aliwasaidia kubeba kombe la Premier League.

Advertisements
%d bloggers like this: