Skip to content
Advertisements

Irene Uwoya achora tattoo inayodaiwa ya bwana mpya

BAADA ya penzi lake na mwanamuziki wa Bongo Fleva, kupotelea hewani, hatimaye Diva machachari kunako tasnia ya filamu Bongo, Irene Uwoya, anadaiwa kunasa penzini kwa mwanaume aliyemchora tattoo anayefahamika kwa jina la Salaah. 

Ubuyu huyo uliibuka baada ya picha ya Uwoya kusambaa mitandaoni ikiuonyesha mgongo wake vizuri uliopambwa na tattoo mbili, moja ya jina la mwanaye Krish na nyingine ya jina la Salaah. 

Picha Msanii Irene Uwoya Akionyesha tattoo inayosemekana ya mpenzi wake mpya


Wachambuzi wa masuala ya ubuyu wanadai kwamba inawezekana Uwoya kafa na kaoza kwa mwanaume huyo ndiyo maana kaamua kumchora mgongoni mwake na kumuanika hadharani, kitu ambacho siyo kawaida yake kwani hata Msami hakuwahi kumuweka hadharani. 

Wachambuzi hao wanaendelea kuperuzi ili waweze kujua huyo Salaah ni nani, ila inasemekana ni jamaa ambaye β€˜chenji’ hazimpigi chenga. 

Advertisements

1 Comment »

%d bloggers like this: