Skip to content
Advertisements

Ratiba ya raundi ya nne kombe la ligi england; man united v swansea .

TIMU ya Manchester United itamenyana na Swansea City katika Raundi ya Nne ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup. 

Hiyo inafuatia ushindi wa 4-1 dhidi ya Burton Albion kwenye mchezo wa jana Uwanja wa Old Trafford, mshambuliaji chipukizi, Marcus Rashford akifunga mabao mawili dakika ya tano 17. 
Mabao mengine ya Man United yalifungwa na Jesse Lingard dakika ya 36 na Anthony Martial dakika ya 60, wakati la Burton Albion limefungwa na Lloyd Dyer dakika ya 90 na ushei. 
Tottenham watakuwa weneyji wa West Ham mjini London, Chelsea watamenyana na Everton Uwanja wa Stamford Bridge, Arsenal wataikaribisha Norwich na Wolves watamenyana na Manchester City Uwanja wa Etihad. 
Kocha mpya wa Crystal Palace, Roy Hodgson atakwenda ugenini kuifuata Bristol City wakati vinara wa Championship, Leeds watamenyana na Leicester Uwanja wa King Power na mchezo wa mwisho Bournemouth wataikaribisha Middlesbrough. 
Mechi hizo zitachezwa Oktoba 23/24 katika tarehe rasmi a muda vitakavyotajwa baadaye kwa kila mchezo. 

RAUND YA NNE CARABAO CUP
Tottenham v West Ham

Bristol City v Crystal Palace

Swansea v Manchester United

Arsenal v Norwich

Chelsea v Everton

Manchester City v Wolves

Leicester v Leeds

Bournemouth v Middlesbrough

Fixtures to be played October 23/24 

Advertisements
%d bloggers like this: