Skip to content
Advertisements

Nikki wa pili amchana dogo janja

STAA wa Hip Hop Bongo, Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’, amempa makavu msanii mwenzake, Abdulaziz Aboubakar Chende ‘Dogo Janja’ kwa kumweleza kuwa anatakiwa kujitambua kwani amekua hivyo ni wakati wa kutathmini maisha yake na kuachana na skendo za wanawake kwani hazina mpango.

Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Nikki alisema, Dogo Janja kwa sasa amekua hivyo ni wakati wa kupanga maisha na kuutazama muziki wake kwa upana zaidi kuliko kuendekeza skendo za wanawake kila kukicha kwani hazitamjenga bali zitambomoa.

“Namkubali sana Dogo Janja ndiyo maana mwaka jana nilisema wazi kuwa ndiye msanii wangu bora, ninaendelea kumshauri bwana mdogo kusimama zaidi katika kukuza muziki wake kwani sasa amekuwa kijana mkubwa, skendo za wanawake hazina mpango, anapaswa kuziacha,” alifunguka Nikki ambaye ni mmoja wa wasanii wanaounda Kundi la Weusi.

Advertisements
%d bloggers like this: