Skip to content
Advertisements

Pogba kutibiwa na Daktari wa Barcelona

Mchezaji wa timu ya Manchester united “Pogba”

Nyota wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba huenda akafanyiwa upasuaji na daktari kutoka Finland Sakari Orava ambaye amefanikisha upasuaji wa winga wa Barcelona Ousmane Dembele. 

Ripoti kutoka kwa daktari huyo ambaye ni mtaalam wa tiba ya misuli zimeeleza kuwa huenda akafanya mazungumzo na Pogba siku ya Jumatatu kwaajili ya kuanza upasuaji ndani ya wiki ijayo. 


Orava amesema atajadili na Pogba ili kuona kama kuna ulazima wa kufanyiwa upasuaji au kutibiwa kwa njia ya kawaida tu kwa kuwa tatizo lake ni dogo ukilinganisha na Dembele ambaye ilikuwa lazima afanyiwe upasuaji. 


Pogba mwenye miaka 24 aliumia misuli ya Paja kwenye mchezo wa Uefa dhidi ya FC Basel Septemba 12 mwaka huu.

Advertisements
%d bloggers like this: