Skip to content
Advertisements

Wabunge Lema na Nassari kuunguruma Takukuru

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, wamesema watakwenda kumuona Mkurugenzi wa Takukuru , Valentino Mlowola ili kumpa ushahidi wao kuhusu tuhuma za rushwa kwa madiwani waliokihama chama hicho na kuhamia CCM.

Lema na Nassari wataenda kutoa ushahidi kuhusu madiwani 7 waliojiuzulu katika majimbo yao wanaowatuhumu kupokea rushwa ili kujiuzulu nafasi zao.

Mh. Lema ameelezaa kuwa Jumatano hii kuwa β€œTutakwenda kumuona Mkurugenzi wa Takukuru na kumpa ushahidi wa biashara mpya haramu ya madiwani,” ametweet .
Kwa upande wake mbunge Nassari ambaye madiwani watano katika jimbo lake wamejiuzulu amekwenda Nairobi nchini Kenya kuonana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kupata baraka zake kabla ya kwenda Takukuru.
Valentino Mlowola ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, alisema kuwa ofisi hiyo inawasubiri wabunge hao kuwasilisha ushahidi wao ili waufanyie kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu.

Advertisements
%d bloggers like this: