Skip to content
Advertisements

Mchungaji Msigwa kizimbani kwa kutishia kuua

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo mjini humo kwa tuhuma za kutishia kuua.

Msigwa anashtakiwa kwa kumtolea matusi na kutishia kumuua diwani wa kata ya Kitwiru, Baraka Kimata.

Wengine waliopandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo ni dereva wa mbunge huyo, Godi Mwaluka na diwani wa viti maalum, Selestina Johanes.

Akisoma mashtaka hayo, hakimu wa mahakama hiyo, Rehema Mayagilo alisema kuwa washtakiwa hao walifanya kosa hilo jana majira ya saa nane mchana katika eneo la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Mchungaji Msigwa na wenzake walikana mashtaka hayo na wakaachiwa kwa dhamana. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Oktoba 9 mwaka huu.

Advertisements
%d bloggers like this: