Skip to content
Advertisements

Zamaradi afunga ndoa Kimyakimya, mumewe awa gumzo

Zamaradi akiwa na mumewe kwenye ndoa yake

Hatimaye mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema amewaacha baba na mama yake na kuambatana na mumewe rasmi katika tukio lililofanyika ‘kimyakimya’.

Zamaradi amevunja ukimya kwa kuweka kwenye Instagram picha ya ndoa yake na mumewe ambaye hakuonekana vizuri sura na kuandika, “ALHAMDULILLAH!!”

Hata hivyo, sura ya mume wa Zamaradi imezua gumzo zaidi mtandaoni kutaka kumtambua, huku wengi wakidai kuwa ni ndugu wa kiongozi mkubwa kwenye Serikali ya Awamu ya Tano.

Pongezi zisizokifani zimemiminwa na wasanii na watu maarufu kwa mtangazaji huyo ambaye ni mama mtoto wa Mkurugenzi wa vipindi na utayarishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

“Ndoa yako iwe ya kheri. Inshallah,” ameandika Faiza Ali ambaye ni rafiki wa karibu wa Zamaradi.

Imekuwa vigumu kwa baadhi ya watu kuamini wakidhani huenda anaandaa filamu yake.

DONDOSHABLOG inampongeza Zamaradi kwa hatua aliyoifikia. Ndoa yake ikawe baraka kwa jamii nzima.

Advertisements
%d bloggers like this: