Skip to content
Advertisements

Dawa nguvu za kiume yauwa 

Mzee mmoja mwenye umri wa miaka 60 amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu ya kuongeza nguvu za kiume kwa mganga wa kienyeji mkoani Shinyanga. 

Kufuatia kifo hicho kwa mzee huyo Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mtu mmoja ambaye ni Mganga wa kienyeji ambaye anatuhumiwa kusababisha kifo cha mzee huyo mwenye umri wa miaka 60 wakati anamfanyia matibabu ya kumuongezea nguvu za kiume kwa njia ambayo imetajwa kuwa sio sahihi. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga amethibitisha kumshirikia mganga huyo na kudai kuwa upelelezi unaendelea na pindi ushahidi utakapokamilika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria. 

Advertisements
%d bloggers like this: