Skip to content
Advertisements

Watu 17 wamepoteza maisha kwenye ajali ya lori Zambia

Watu 17 wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine 48 wakiwa wamejeruhiwa vibaya katika ajali ya lori kusini mwa Zambia.
Ajali hiyo imetokea baada ya lori kupinduka.
Kwa mujibu wa habari,dereva wa lori hilo alikuwa akiendesha kwa mwendo wa kasi sana wakati lori hilo likipinduka katşka kijiji cha Kasimango.
Ripoti zinaonyesha kuwa wote waliopoteza maisha ni waumini wa kikatoliki waliokuwa wakielekea katika milima ya Senga kwa ajili ya shughuli za kanisa.
Polisi katika eneo hilo wanasema kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka kutokana na majeraha makubwa waliopata abiria.

Advertisements
%d bloggers like this: