Skip to content
Advertisements

Mbatia atoa tuhuma nzito

Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amesema kuwa zipo njama chafu za kumdhuru na kutengeneza ushahidi wa video na picha mnato na kuzisambaza. Mbatia alidai kuwa njama hizo alizozigundua zilipangwa katika mikakati tofauti na kuhakikisha zinafanikiwa
Mbinu ya kwanza iliyopangwa kutumika kuwa ni kumteka akiwa anaelekea nyumbani kwake au mahali popote. Mbinu ya pili alidai kuwa ni kuwapandikiza na kuwavisha vijana sare za Chama cha Chadema, ambao wangemvamia mahali popote, wamteke na kumjehuri ili ionekane kuwa ndani ya Ukawa kuna mgogoro.Ya tatu kwa mujibu wa Mbatia, ni kuwakusanya wajumbe wa chama chake na wanachama kwa pamoja ili waende kumfukuza kwenye Chama, kwa madai ya kutotekeleza majukumu yake ipasavyo.

Advertisements
%d bloggers like this: