Skip to content
Advertisements

SWIZZ BEATZ NA DIAMOND PLATNUMZ MAMBO YANAIVA, USHAHIDI MWINGINE WAJITOKEZA

Staa na mtayarishaji wa muziki kutoka Marekani Kasseem Dean a.k.a Swizz Beatz amekumbushia ukamilishaji wa kolabo ya kimuziki kati yake na Staa wa Bongo Fleva ‘Diamond Platnumz’ katika ujumbe wake wa kumtakia siku njema ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.
Kupitia video aliyoweka Diamond Platnumz katika ukurasa wake wa Instagram inayomuonesha Dj kutoka kituo cha 99JAMZ kilichoko Miami, Marekani akichezwa wimbo wa ‘Hallelujah’ ft. Morgan Heritage post hiyo mbali na maoni ya mashabiki juu ya hatua hiyo ya mapokezi ya wimbo, Swizz Beatz alituma ujumbe katika uwanja wa maoni akimtakia siku njema ya kuzaliwa kwake na kushindilia juu tamanio la kukamilika kwa kolabo yao ya pamoja.

Ujumbe huo wa Swizz Beatz ulipokelewa vyema na mashabiki wa muziki wa Tanzania huku wakionesha utayari wa kuipokeza kazi hiyo ya pamoja hata wengine wakimkaribisha kwa hamu nchini Tanzania.

Advertisements
%d bloggers like this: