Skip to content
Advertisements

Simulizi ya “Regret” sehemu ya kwanza 

Naitwa Samia wengi walipenda kuniita Sami mi pia Nilikua napenda kuitwa ivyo,Nilikua mtoto wa kwanza kwa Mamangu, Ingawa Baba sikujua kama alimfukuza mama au Mama aliondoka mwenyewe Kwani kwa muda huo Nilikua Nikiishi na mama wa kambo(Ma mdogo).

    Ilikuwa asubuhi siku ambayo kulikua na baridi kali nilikua bado nimelala niliposhituka na kukuta kumbe nimelowanishwa na maji tena yalikuwa ya baridi hasa yakiwa yameambatana na barafu.Sikuuliza kitu bali nilikutana na maneno tu 
“Hivi weee Kahaba mpaka sasa hivi umelala nani akufanyie kazi za hapa ndani eeeh?? Na kama mama yako alikudekeza hapa umeingia choo cha kiume pumbavu weeh, na nikirudi utajuta kwa nini baba yako kanioa mie” Nilimtizama kwa umakini bila hata ya kutia neno huku nikitetemeka na kuhisi baridi.
Niliyafuta macho yangu kwa vidole huku mwili ukionekana kuchoka sana,nikajinyanyua kiuchovu Ma mdogo akaniletea nguo zake pamoja naza baba.

Nilifurahia kuona nguo za baba yangu lakini nilichukizwa na nguo za Ma mdogo.Sikupenda sana nilijua kuwa ananitafutia sababu tu kwa baba.Nilifua na kufanikiwa kumaliza japo kwa shingo upande.Alipika chakula tukala, Ma mdogo alikua akinitesa sana ila ndani ya Nafsi yangu nikajisemea Itanibidi kuvumilia kwani nimebakiwa na muda mchache wa kurudi shuleni.

 “We kahaba unaenda wapi” ma mdogo alilongea ,kiukweli lile jina la kahaba huwa linaniumiza na kuniuzi kwani mpaka nimefika umri wa kuvunja ungo simfahamu mwanaume iweje leo naitwa kahaba??? Nilitamani kumwambia baba,ila moyo ulisita kwa kuelewa kuwa katekwa na mapenzi mpaka kumfukuza mama na kumleta Yeye, Basi Nikamjibu
“Naenda kulala”nilimjibu japo kwa unyonge sana Akaniambia “Mi natoka,naenda kwenye mihangaiko yangu ila nikirudi nikute umepika Chakula cha Usiku sawa??” 

Nikajibu “Sawa”…. 

Niliingia kulala wala sikupatwa hata na chepe la usingizi bali nilijikuta katika dimbwi zito la mawazo,sikujua ni kwanini Wakati huo na waza nilisikia sauti ikitawala kichwani mwangu kwa kuniongelesha “Mwanangu nakupenda sana,sikupenda kuondoka kwa baba yako lakini kwa manyanyaso aliyo nipatia,Ndo nikaamua kuondoka mie,Naomba usome kwa bidii ili uje kunisaidia mimi na wadogo zako akina Janeth na Josia”           

nilijihisi kuishiwa nguvu “hivi ninaota au nimepatwa na kitu gani?” Nilichukua kidonge cha hedex kwa kutuliza maumivu kwani kichwa kilinigonga sana.Ikanibidi kuingia jikoni na kuanza maandalizi kwaajili ya mlo wa usiku.Kila kitu kilikwenda sawa na muda nao uliyoyoma bila Ma mdogo kutokea licha ya baba kusafiri kwenda Dar kikazi.
Nyumba nilianza kuiogopa kwani nilibaki peke angu afu na ma mdogo anachelewa kurudi Niliogopa sana, 

“ng’o ng’o 

ng’oooo,

mpuuzi weee fungua,unanichoresha hapa nje sioo?,utalala nje wewe sio Mimi 

Embu fungua au nibomoe huu mlango na kesho niutengeneze mpya?..” 

zile kelele zilinifanya kuamka kwani nilikuwa na usingizi,hakika usingizi ni sawa na kifo japo sijawahi kufa bali ni usemi tu wa wahenga husema hivyo.
Nilifungua mlango na sikuamini kilichonikuta baada ya kukutana na kikumbo na matusi ambayo sijawahi tukanwa na kama nikikusimulia hapa unaweza kulia,nilijikaza ila cha ajabu ma mdogo alikuwa kashikwa kiuno chake na mwanaume ambae huwa anatuletea maji ya matumizi ya nyumbani kama ya bomba yakiwa yamekatika tena alipitiliza nae hadi ndani Nilibaki Nimeacha Mdomo wazi Mana mi nilijua labda anamsindikiza tu

Ma mdogo jwa ukali akanambia

“Ole wako ukija kumwambia baba yako nakunyongaah!!” Nililia sana kwa kuona vitendo ambavyo havinipi utukufu mbele ya macho yangu. 
  Tena walienda Chumbani ambako ma mdogo huwa analala na baba Niliwaza sijui nifanyaje

Mana baba alikua mbali na sio wa kurudi leo wala kesho ndomana ma mdogo akawa huru kufanya udhinifu wake tena bila aibu mbele yangu haikua mara ya kwanza ila siku hiyo nilistajabu kuona hadi mbebe maji anakua nae…..

Itaendelea…

Advertisements
%d bloggers like this: